JINSI INTERNET INAVYOFUNGWA.
Katika Kila Nchi huwa ni makampuni yanayotoa huduma ya Internet kutekeleza maagizo ya serikali ya kubana mtiririko wake kihuduma.
Mfumo mmoja unaotumika kuminya matumizi ya internet unafahamika kama "URL-based blocking" ambapo huwa wanazuiwa viunganisho fulani kwenye mtandao.
Huu ni mfumo unaohusisha kuweka kizuizi , kama kichujio hivi kinachowazuia Wateja kuingia katika mitandao iliyopigwa marufuku.
Mteja anayejaribu kuingia katika mitandao hiyo hupata ujumbe "Server nof found" (Sava haipatikani) au "Tovuti hii imezuiwa na msimamizi wa mtandao".
Mfumo mwingine unafahamika kama "Throttling", kwa maana ya kubana na kunyonga internet.
Mbinu hii ya kuzuia kiwango kikubwa cha idadi ya Wateja wanaotwmbelea mtandao fulani, na kutoa hisia kwamba Kasi ya huduma ni ndogo na kuwafanya Wateja wqelekee kwingine.
Mbinu hii huwa vigumu kwa anayetumia mtandao kubaini kwamba inafanyika kwa sababu ni vigumu kubaini iwapo mitandao inazuiwa wazi au kupunguza kwa kasi ya mtandao ni kutokana na upungufu wa miundombinu (ndiyo maana hapo ulipo unasema "mtandao unasumbua", mara unasema "Leo network iko chini". Mara utasema "yaani mtandao haupatikani". Pole.)
Kama hatua ya mwisho ya kampuni za Mawasiliano zinaweza kutakiwa kufunga kabisa huduma ya Internet kwa ujumla na kuzuia Wateja kupokea data yoyote.
Dola yoyote Ina uwezo wa kudhibiti kampuni ya Mawasiliano kwa sababu vibali vyao vinatokana Dola husika, hivyo wanaweza kutozwa faini au kunyimwa kibali iwapo watakataa maagizo ya Dola ya kudhibiti internet.
Kampuni za Mawasiliano zinaweza kukata Rufaa Mahakamani lakini uhalisi ni kwamba haki ya kampuni za Mawasiliano haipatikani katika mazingira hayo.
Kulingana na Shirika la ACCESS NOW linasema mwaka 2019 kulikuwa na matukio 213 ya kufungwa internet. Mwaka 2018 kulikuwa na matukio 188 na mwaka 2017 yalikuwa 106. Hii Ina maana lipo ongezeko kubwa la kuminya huduma za internet barani Afrika, huku serikali zenyewe zikijikosesha mapato.
Twenzao 🏃 🏃
DAMYGASO TECH SOLUTIONS
ELEVATING TECH BEYOND LIMITS
0 Comments