JINSI YA KUIFANYA BLOG au WEBSITE IPATIKANE KWENYE SEARCH ENGINE KAMA GOOGLE

Unaweza ukawa ushawahi kusikia Search engine (Injini ya utafutaji) lakini hukuwahi kuielewa mpaka muda huu unaposoma chapisho hili.

👉Injini ya utafutaji ni mfumo wa programu ambao umeundwa kutekeleza utafutaji wa wavuti. Inatafuta Wavuti Ulimwenguni kote kwa njia ya kimfumo kwa habari fulani iliyobainishwa katika swali la utafutaji wa maandishi. 

👉Mfano ukiandika jina lako kupitia Google ukasearch lazima zije akaunti zako za social media ambazo umezifungua Kwa jina lako na kama hauna akaunti kama hizo suggestions itakayotokea hapo ni NECTA results, nenda kajaribu uone.

👉So kazi ya Search engine yeyote iwe google au nyingineyo ni kutafuta web/ blog yako popote ilipo au kutafuta post ulioiandika popote pale ilipo. Hata hivyo Huwa inatokea search engine inashindwa kuona hiyo blog yako au post yako. Hivyo utahitajika kuisaidia kujua namna ya kupata blog hiyo au post yako. 

👉Zifuatazo ni njia za kuifanya blog au website yako ionekane kwenye search engine:-

1️⃣Ruhusu blog yako ionekane kwenye search engine. 

Hii ni Kwa wale wanaotumia blogger ambapo kuna mambo kadhaa wanatakiwa kuyafanya kwenye settings. 

👉Mambo hayo ni:-

Ingia kwenye setting utaiona kwenye menu upande wa kushoto kisha kwenye kipengele cha Privacy kuna palipoandikwa "Allow search engines to find your blog" washa hicho kibatani.

Then Kwenye hiyo setting shuka chini kuna palipoandikwa Crawler and indexing washa hicho kibatani kilichoandikwa "Enable custom Robot.txt" 

Kwa wale ambao wanatumia wordpress ama website zao huna haja ya kufanya jambo lolote zaidi ya kusubiri hatua inayofuata. 

👉Jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa blog au website yako haihitaji password ili kuweza kuifikia. Au kurasa ambazo unahitaji zionekane kwenye search engine hazihitaji mtu kulogin.

2️⃣Isajili blog au website yako kwenye search engine. 

👉Karibia search engine zote kubwa zina mfumo wa kuisajili website au blog yako. Kwa mfano 

🔹 Google wanatumia Google Search Console, 

🔹 Microsoft bing wanatumia Bing Webmaster Tools,   

🔹 Yandex wanatumia Yandex Webmaster n.k. 

Unachotakiwa kufanya ni kujisajili kwenye hizo search engine. Kwa mfano ukitaka kujisajili Google search console unaweza kubofya link hii HAPA 

Utalog in kwa email yako, kisha Utatakiwa kuweka link au domain ya blog au website yako

Kama hujanunua domain, weka link ya blog yako hapo palipoandikwa URL prefix.

So kama una website au blog usije ukaona suala la ku.rankup kwenye search engines linakuwa gumu kwako ukahisi Kuna mkono wa mtu😂

Inatakiwa ufahamu hivi vitu hapa

👉Indexing 

👉Crawling 

👉Breadcrumbs 

Kwa kuvisoma zaidi BOFYA HAPA

Twenzetu 🏃🏽‍♂️🏃🏽‍♂️

ELEVATING TECH BEYOND LIMITS

FOLLOW US FOR MORE

Post a Comment

0 Comments