👉Katika ulimwengu wa leo, kujua kutumia kompyuta na simu janja ni ujuzi wa lazima. Hata hivyo, kozi hizi mbili zina malengo na upeo tofauti. Lakini kozi ya kutumia simu janja imepuuzwa sana kwasababu watu wamekuwa wakichukulia simple kuhusu suala Zima la kujifunza kutumia simu.
👉Kwa tafiti zangu ambazo hazijatimia, sijafanikiwa kuona kituo au sehemu inayofundisha jinsi ya kutumia simu janja na sina hakika kama kweli watu hawana uhitaji wa kujifunza. Ila Nina hakika kupitia movements ninazoziona kuwa Kuna ulazima wa kuwafundisha watu jinsi ya kutumia simu janja.
👉Kujifunza kozi ya jinsi ya kutumia kompyuta sio vibaya, ila lengo langu na lengo la Kila mtu ni kutokufanya vitu Kwa ugumu.
Wazungu wanasema "work smart, not harder". Kumbe sasa, kozi ya kutumia simu janja ndio msingi ambao utakurahisishia wewe unayejifunza kutumia kompyuta uweze kufanya vitu kuwa rahisi na Kwa haraka zaidi.
Maswali ambayo unaweza ukawa unajiuliza 👇🏿
❓Je unajua kutumia simu janja?
❓Je una Kila sababu ya kutaka kujua kutumia simu janja ipasavyo ili ikurahisishie shughuli zako?
Au
❓Unaridhika na matumizi Yako ya simu janja Kwa sasa?
👉Sababu kubwa ya kufikiria kuanzisha smartphones course ni kwasababu asilimia kubwa tunatumia smartphones na Kuna vitu tunashindwa kuvifanya tukiamini kuwa inabidi tuwe na kompyuta ndo tuweze kufanya.
👉Kuna maswali ambayo Huwa naulizwa, na kabla ya kuyajibu Huwa nafikiria mara mbili mbili kwasababu ni maswali ambayo napaswa niulizwe na mtu ambaye hana smartphone. Thus why waliotengeneza simu walisema kuwa "SMARTPHONES IS FOR SMART PEOPLES"
❓Je na wewe upo kwenye list ya hao smart peoples?
👉Hebu tuangalie kwa undani Nini unaweza ukajifunza kwenye hizi kozi mbili:
💻 COMPUTER COURSE
Maudhui Unayojifunza
👉Misingi ya matumizi ya kompyuta (Word, Excel, PowerPoint).
👉Ujuzi wa intaneti na barua pepe.
👉Jinsi ya kushare mafiles online na offline (wireless & wired)
👉Mfumo wa uendeshaji (Windows, Linux).
👉Mambo ya kitaalamu kama programming, web development, graphics design, cybersecurity n.k.
Lakini wengi mnaoenda kusoma computer course mnaishia kujifunza hivo vitu viwili vya mwanzo
Faida za kujifunza computer course
👉Hutoa fursa kubwa za ajira na ujuzi wa kitaalamu.
👉Kompyuta zina uwezo mkubwa wa kuchakata data na kutengeneza programu.
👉Ni msingi wa teknolojia nyingi kubwa duniani.
📱SMARTPHONE COURSE
Maudhui Unayojifunza
👉Misingi ya kutumia simu janja (kuwasha na kuzima, kutuma na kupokea ujumbe, kupiga na kupigiwa, kuchaji).
👉Jinsi ya kutuma na kupokea mafiles online na offline
👉Ujuzi wa intaneti na barua pepe.
👉Jinsi ya kutengeneza Google account & Apple account ili kupata access ya kutumia play store na app store
👉Kutumia apps maarufu kama vile (WhatsApp, Facebook, Instagram, Telegram).
👉Malipo ya kidijitali (mobile money, banking apps).
👉Usalama wa simu na matumizi ya cloud storage.
Faida za kujifunza smartphones course
👉Ni rahisi na inapatikana kwa kila mtu.
👉Inarahisisha biashara ndogo na masoko mtandaoni.
👉Husaidia mawasiliano ya haraka na huduma za papo kwa papo.
👉Inasaidia kupata utatuzi wa changamoto ndogox2 za kiteknolojia
ULINGANISHO ULIOPO KATI YA kati HIZI KOZI MBILI
1️⃣Computer Course inajumuisha teknolojia pana na ya kitaalamu kama vile uchambuzi wa data, utengenezaji wa programs n.k
Lakini
Smartphone Course inajumuisha Matumizi ya kila siku ya simu kama vile mawasiliano, malipo, burudani na masoko mtandao
2️⃣Computer Course Inahitaji muda na umakini
Lakini
Smartphone Course Ni rahisi kujifunza na Kwa haraka zaidi
3️⃣Computer Course Ina fursa za ajira Nyingi (ofisi, IT, uhandisi)
Lakini
Smartphone Course Ina fursa za ajira chache (digital marketing, biashara ndogo)
4️⃣Computer Course Inahitaji gharama kubwa zaidi ya kujifunza
Lakini
Smartphone Course inahitaji gharama ndogo ya kujifunza, japo sijapata experience ya kuona mtu akifundisha
Kwa hiyo, kozi zote mbili ni muhimu kulingana na malengo yako
👉Ukihitaji taaluma na ajira kubwa
Computer Course inakufaa.
👉Ukihitaji ujuzi wa matumizi ya haraka na biashara ndogo,
Smartphone Course ndio chaguo lako.
❓Je upo tayar kujifunza course mojawapo kati ya hizo?
Kwa kujifunza BOFYA HAPA na uandike nipo tayari kujifunza
Na kama unataka kuona fursa zilizopo kwenye ulimwengu wa teknolojia BOFYA HAPA
Usisahau kushare Kwa wengine ili wajifunze pia
ELEVATING TECH BEYOND LIMITS

0 Comments