Ukiangalia kwenye chapisho lililopita la MAANA YA ULIMWENGU WA TEKNOLOJIA , utaona kuna vitu vinne ambavyo ndio msingi mzima wa jinsi ulimwengu wa kiteknolojia unavotenda kazi.
1️⃣kitu cha kwanza ni ubunifu na uvumbuzi, ambapo maini character na starring katika part hii ni binadamu, yaani wewe.
2️⃣kitu cha pili ni vifaa, ambapo sisi tunazungumzia zaidi vifaa vya kielektroniki ambavyo ndo vichochezi Vikuu vya utandawazi.
3️⃣kitu cha tatu ni program na mifumo. (Utaratibu)
4️⃣kitu cha mwisho, ni sekta mbali mbali (maisha halisi).
So utendaji kazi unakua hivi,
👉 ubunifu na uvumbuzi unakua unao wewe mwanadamu. So unachohitaji ni vifaa na namna ya kuvitumia ili uweze kubuni na kuvumbua vitu.
❓Je, hivi vifaa vinakua na nini?
👉 Kwenye hivi vifaa unavovihitaji wewe ndo vinakua na program au mifumo mbali mbali inayotumika kuendesha hivo vifaa.
❓Je unatumia hivo vifaa na hiyo mifumo kufanya nini?
👉So, wewe ambaye ndiye umebeba teknolojia, unatumia hivo vifaa na mifumo, kuja kuanzisha sekta au kuboresha sekta.
❓ Kwani sekta ni nini?
👉Sekta ni mgawanyo wa shughuli za kiuchumi au kijamii kwa ajili ya utaalamu maalum. mfano tuna sekta ya afya, sekta ya elimu, sekta ya biashara, n.k.
So, unaweza ukajiuliza swali la ufahamu
❓ kati ya sekta na teknolojia kipi kilianza.
Ambapo Ni sawa na kusema
❓ kati ya maisha unayoishi na wewe mwenyewe nani alianza.
👉Kiufupi ni kuwa teknolojia ndiyo ilianza, na sekta zikafuata baada ya watu kuanza kuhitaji mgawanyo wa shughuli na utaalamu.
Uhusiano kati ya sekta na teknolojia
✅Teknolojia huzaa sekta mpya.
✅Sekta hufanya teknolojia kukua zaidi kwa kuhitaji ubunifu na uboreshaji.
Nikirejerea nilipokuwa kidato Cha nne Kuna mada tulisoma kwenye somo la civics ambayo ni utandawazi (globalization).
❓Je utandawazi ni nini?
👉Utandawazi ni mchakato wa dunia kuunganishwa na kushirikiana kwa karibu kupitia teknolojia, biashara, mawasiliano, utamaduni na siasa.
Na Ile maana fupi tuliyokuwa tukiipenda wengi kwasababu ili turahisishia kukariri ni
👉 utandawazi ni hali inayofanya dunia kuwa “kijiji kimoja”, ambapo mipaka ya kijiografia haizuii tena watu kushirikiana au kubadilishana rasilimali.
❓Swali la kujiuliza ni kuwa nawezaje kuishi kwenye uwepo ambao utanifanya nione dunia kama Kijiji kimoja ilihali hata makao makuu ya mkoa nilipo siyajui?
Ili kupata jibu, itabidi urudi kwenye utendaji kazi wa ulimwengu wa teknolojia hapo juu ambapo ndani yake Kuna vifaa vya kielektroniki na program/mifumo.
👉So kupitia vifaa vya kielektroniki na programs zake, hapo ndipo unaweza ukawa na uwezo wa kuifeel Dunia kama Kijiji kimoja.
Kumbe Sasa, vifaa vya kielektroniki vilianzishwa ikiwa kama driving force of globalization na hiyo ndiyo kazi yake kuu.
Nitajibu swali ambalo nililiandika kwenye chapisho lililopita, ambalo liliuliza
❓Kwanini ninakuelezea kuhusu ulimwengu wa kiteknolojia?
👉Kilichonifanya niandae makala hii ni baada ya kufanya tafiti na kugundua zaidi ya 80% ya watanzania hawajui kutumia smartphones na computers, bali wamejikuta wakiishia kufanya show business. Kwamba inabidi awe na smartphone ili watu waone na yeye hajaachwa nyuma, yupo bampa to bampa na TECH.
Hapa chini Kuna maswali ambayo Huwa napenda kuwauliza watu ambao wanakuja na changamoto ambazo naona ilibidi wazitatue kupitia smartphones zao. So Sasaiv naweza nikakuuliza hata wewe unayesoma makala hii
❓Je unajua kutumia smartphones?
❓Je una sababu za msingi ambazo unaweza ukazitumia kunishawishi Mimi ninayetumia kiswaswadu ili ninunue smartphone?
Kama majibu Yako unaona Yana utata basi na wewe bado haujui kutumia smartphones.
Kama unataka kujifunza kutumia smartphones unaweza KUBOFYA HAPA na baada ya hapo uandike nahitaji kujifunza
USHAURI
Kwa watu ambao nishakutana nao face to face, Huwa ninashauri kabla ya mtu kwenda kujifunza computer course inatakiwa afundishwe smartphones course.
Kabla hujaenda kuitafuta smartphones course, nitakuelezea kwanini smartphones course kabla ya computer course....
Usisahau kushare Kwa wengine ili wajifunze pia
ELEVATING TECH BEYOND LIMITS
0 Comments